Home INSTRUMENTALS SIMULIZI | KISICHO RIZIKI AKILIKI

SIMULIZI | KISICHO RIZIKI AKILIKI

Nakumbuka kipindi kile miaka ya 1990, nikiwa nimechoka wakati natoka kufyatua toafali aina ya blocks nikitembea barabarani kurudi kwangu nyumbani nikiwa na kiu kuu na njaa, jua likiniwakia mwili wote ukiwa umechoka, ukipita na Gari yako aina ya BMW huku ukinitimulia vumbi bila huruma. Nilikuwa nakupenda sana na rafiki zangu walijua hilo ila wakasema mimi sio wa aina yako niliwabishaia na kusema mapenzi ya kweli hayajali mali wala uwezo na kuwahaakikishia kuwa lazima nikupate.

Siku ile nikakufata hukutaka kunisikiliza, nilkata tama ila naiakjipa moyo kuwa lazima ipo siku nitakupata, sasa ulionesha waziwazi kiasi gani wanichukia kwa kuniita kinyago, nilijua ulikuwa uanfanya kazi bank na ulikuwa na nyumba nzuri na Gari zuri ila sikulegeza kamba na sikuogopa nilizidi kukupenda Jakie.
Siku ile ulikuja sokoni nilikuja na kuomba kuongea nawe nilikueleza kuwa nakaupenda, hukujali nilizidi kusema, ukaamua kuniitia watu kuwa mimi ni mwizi nataka kukuibia Gari! Mimi niwe mwizi hata kuendesha baisjkeli sijui, iliniuma sana. Walinipiga mpaka nikalazwa hospitali nikiwa sina msaada kwani mama na baba yangu walikuwa walisha kufa kitambo na kuniacha mimi tu nikiwa yatima. Ila ulinihurumia na kuja hospitali, nilitabsamu nilipokuona, ulinomba msamaha kwangu nilkuwanishakusamehe, nakumbuka nilikuambia neno hili, “Nakupenda sana Jakie” ulilia machozi nikajiakaza kuamka japo maumivu yalikuwa makali nikakufuta machozi Jakie…..

Nakumbuka siku ile ulivonambia unataka kuja kwangu. Nilistuka sana mpka ukashangaa, ndiyo nilistuka sana kwa kuwa hadhi yako ilikuwa haiendani na ninapokaa mimi. Nilikukatalia ila ukasisitiza kuja, nilikubali na tukaanza safari ya kuktaisha vichochoro mpaka nilipokuwa nimepanga, kwa uzuri wako hukustahili kuingia pale, ila ukakubali tayari moyoni nilijua kuwa umenipenda na unanijali… sasa tulifika, chumba change kilikuwa kidogo mno, godoro la inch 3 tena bila kitanda, sikuwa na vitu vingi na chumba hakikuwa na umeme, niliiona huzuni usoni mwako sikusita kusema kwa sauti ya upole nay a kuumiza
‘Jakiez mpenzi wangu, mimi nakaa hapa hii ndio hali halisi ya maisha yangu, naomba tu uvumilie!” niliongea kinyonge ulishuka na kukaa kwenye godoro, ukaomba glass kwajili ya kunywa juis uliyoniltea kama zawaidi, sikuwa na glass bali kikombe kikubwa cha bati…nilikupa ukamimi na kuninywesha, kwangu ilikuwa siku ya kipekee na ya Furaha ytangu nizaliwe ktk hii dunia nilikunywa nikakunywesha. Ulikuwa upendo mkuu mno kwetu mimi na wewe kwa furaha nilitoa machozi mimi Samuel Marc, ukaniuliza walilia nini? Sikujibu badala yake ukanikumbatia na kunifuta machozi, nilikukumbatia pia, hukusita Jackie uakalala kifuani pangu, hii ilidhihirisah umekubali ombo langu la kuwa wachumba, niliziidi kufurahi. Uliinuka na kunikumbatia kwa nguvu nikafanya hivo, sikujua kipi kilinifanya nikukumbatie ila sasa nilihisi mwili wako ukitetemeka na ukanimabia masikion mwangu:
“Sam Nakupenda sana tafadhali nismehe yote nakupenda sana”
“nakupenda zaidi pia nilishakusamehe mda mrefua” nilijibu. Sasa tulizidi kukumbatiana na sikuelewa kipi kilivua nguo zetu, nilijikuta kama nilivo na wewe kama ulivo miili yetu ya moto ikigusana, nilistuka nikakutoa kifuani huku ukihema kwa kasi;
“Jakie siwezi kufanya chochote kwakuwa hujawahi, kwahiyo kama wanipenda nivumilie mpka niwe na uwezo nikuoe!”
“sawa nimekubali, ila hakikisha unatimiza uliyoseama”
“Nitafanya hivyo usijali mchumba wangu Jakie” nilisema na kusimama kwa aibu nikachukua nguo zake na kumvika na nikavaa zangu. Kisha Jakie akanikumbatia kwa nguvu huku akisema ananipenda sana… akiwa bado kanikumbatia mara mlango uligongwa kwa nguvu nilijua alikuwa ni baba mwenye nyumba, nilimuachaia Jakiez na kwenda kuitika baba alikuw ana hasira sana
“yaani wewe hujalipa kodi ila unahela za kuleta wasichana humu ndani sio, sasa leta kodi hapa laasivyo nawafungia ndani”
“Mzee nitakupa saizi sina”
“Hapana nataka hela hii nyumab si ya babako sawa ehhh”
“Mzee kesho nitajitahidi”
“kila siku kesho kesho kesho haziishi usipotoa utakuatana kigodoro chako huko njiani maana hata niseme nikiuze siwezi kuapata hata mteja wa sh 100” “Sawa mzee mia naitajitahidi kesho nikupe”
Aliondoka nikaingia ndani na kukmkuta Jakiez akiwa kanuna, nilijua amesika yote kwani mzee mwenye nyumab aliongea kwa gahabu kweli. Jakie aliniuliza: “unadaiwa shi ngapi?”
“Ni elfu 12 yani kila mwezi elfu 2 na anataka ya miezi 6”
“Nitakulipia hiyo kodi mpenzi” niliona aibu kukubali kisha akatoa elfu 30000 na kunipa, nilimshukuru sana
“usijali hizo zitakazo baki zikusaidie, pia kuna kitu kizuri nitakwambia!” Kwa tambo nilitoka nje na kumuita mwenye nyumba na kumlipa hela zote nakumbuka nilimwambia 1000 namwongezea ya kunivumilia, baba alifurahi na meno yote yalikua nje ukijumlisha na mapengo yake…
Tulitoka nikakusindikiza mpaka karibu kwenu na kurudi kwangu, sikupika siku hiyo, nilirudia kuhesabu zile hela amenipa kwa kweli zilikuwa nyingi, nilala kwa furaha sana hasa kutoka na Jakie kukubali niwe mchumba wake…

**************Miezi kadhaa baadae***********
Mpenzi wangu Jakie alikopa pessa bank, kwa kuwa alikuwa anafanya kwenye moja ya bank za hapa mjni. Alikuja kwangu na kunielekeza kuwa anataka niachanaena kazi za suluba ili anifungulie duka ila hakujua duka liwe la nini. Nilipendekeza la kuuza vaifaa vya ujenzi, alinisifia na kusema nimechagua vizuri ila akanisisitizia kuwa makini pindi nitakapoanza kuuza kwani pesa alikuwa amekopa na zinatakiwa kurudishwa, alinifundisha namna ya kufanya biashara na tulifungua duka likapewa jina la “SAM Enterprises”. Niliuza kwa umakini mno na baada ya miezi tulifanikiwa kurudisha mkopo na duka likawa linajiendesha lenyewe… baadae tulifungua mengine mengi na hatimaye tukajenga nyumba…. Nakumbuka harusi yetu jinsi ulivokuwa umependeza, tukiwa na wafanya bishara mbalimbali hapa mjini, hakika ulipendeza sana tena zaidi ya sana, tulimaliza harusi na kwenda honeymoon au kama wanavyoita Fungate, kule ndio ulinionesha kunijali, kwani kila nilipojaribu kukuonesha ulimwengu wa ndoa na mahaba Mjomba wangu alishindwa kabisa kusimama.
Ulilia sana, nilijua ulihitaji kwa kuwa tulivumiliana kwa muda wote, nilikusihi uvumilie kwa upendo huku ukinitia moyo ulikubali. Siku nyingine tena tulijaribu hali ikawa ileile, yani jogoo hakuwika kabisa, sasa ulionesha kuchukia, uzuri wako ulipotea na uso wako ulijaa hasira tupu, Nilikubembeleza ukakubali. Niljiona dhaifu sana, sikujua kwanini, jioni ile nikatoka na kukutana na mzee mmoja, nilimueleza tatizo langu, kirahisi tu akaniammbia ninafuraha iliyozidi hivo nitakuwa kawaida, niliona kma anatania nikaamua kurudi kule hotelini kwetu.
Nilikukuta ukiwa umejikunyata kando ya kitanda kwa huzuni, sikuogpoa tena nilikukumbatia na sasa nilijishangaa, jogoo alijibu kwa kuwika tena kwa sauti kubwa kiasi cha wewe kushangaa, mimi na wewe tulikuwa katika ulimwengu mwingine. Japo tulikuwa wageni katika tasinia ya mapenzi ila kila mmoja alifurahi na kufika katika kilele kirufu cha mlima wa Afrika Kilimanjaro. Honeymoon sasa ilikamilika kila mmoja akiwa na furaha tele ***************************************************************
Miaka kadhaa baadae…
Tuliishi kwa upendo na sasa ulikuwa na ujauzito. Nilifurahi ukafurahi zaidi, nakumbuka tulivokuwa tukitaniana eti mtoto atakuwa wa kike au wa kiume! Yote yale yalikuwa mapenzi, kila mtu aliaona chaguo lake ni sahihi mimi nikipenda awe wa kiume na wewe ukipenda awe wa kike. Mungu si athmani miezi tisa ikafika.
Mtoto akazaliwa, yes alikuwa wa kike tukampa jina Catheline, lilikuwa jina zuri, ulifurahi mno mke wangu Jakie, nilifurahi pia hasa kuitwa baba Cathe kama wengi walivyopenda kufupisha. Tulimlea kwa upendo hakuna alichokosa na biashara zetu zilizidi kupanuka zaidi… sasa tulikuwa matajiri wakubwa pale mjini….hii yote naikumbuka, hivi ni mimi kweli? Catherine alikuwa akaanza shule. Mke wangu Jackie ulikuwa huru sasa kufanya kazi zetu. Toka nimekufahamu hukuwa mtu wa marafiki sana, sasa ukaja na rafiki ukinitambulisha kama Janeth. Kidogo nilishangaa kwa kua toka nikufahamu kipindi kile nikiwa nakaa kwenye kijumba kama stoo hukuwahi kuwa na rafiki, ila sikutilia maanani sana, niliona kawiada tu. Miezi ulipita kila mara ukidai kwenda kwa Janethi rafiki yako, sasa hata kuimba kwaya ulikuwa huendi, siku nyingi uliishia kwa Janethi. Nilikuelekeza ila hukunielewa kabisa, kuna wakati ulikuwa mkali sana mpaka nikiwa naogopa.

K Nakumbuka siku ile ulipoaga Kuwa uanaenda kwenye sherehe ya rafiki yake na Janeth, ulituachaa mimi na Catherine nyumbani, ulienda bila gari. Nilikusuburi sana hukutokea kabisa, kwa jinsi nilivyokupenda sikuweza hata kulala. Ilikuwa saa nane, nikimuangalia mwanetu aliyekuwa kalala fofofo. Nilisikia honi ya gari nje, sikusita nikatoka, sikuamini kuona ukishushwa na mwanaume na kukuacha pale ukiwa hujielewi na kabla sijauliza neno gari lile liliondioka kwa spidi. Janeth mke wangu ulikuwa huwezi kutembea mwili wako ulinuka pombe, nilikukokota kwa shida, nilikufikisha ndani hata kupanda kitandani ulishindwa, nilikupandisha nikakuvua viatu, ulianza kutapika pombe harufu ililkuwa kali sana ulimtapikia mwanaetu Carthe kitanda chote ulikichafua. Sikuwa na jinsi zaidi ya kuchemsha maji na kwenda kukuogesha, kubalilisha kitanda na nilifanya kwa umakini mwanetu asijue. Sikuwa na raha hata lepe la usingizi sikulipata ila wewe ulilala fofofo……

Kulikucha hukuonekana kujali, pengine hukukumbuka hata ulichokifanya, nilikuuliza ulinshangaa tu uligeuka ugomvi na ulikuwa mkali kama mbogo alijeruhiwa na simba ukasema ukiondoka huwezi rudi kwani nakunyima raha, akilini nilijua ni hasira na unatania. Nilienda kuoga pekee, hukutaka tena kuoga na mimi kama zamani badala yake ulikuja bafuni na kuchukua taulo langu na kunifungia huko, nilijaribu kutoka ilishindikana, sikuwa na simu wala nini nilisubiri mpaka Cathe arudi ndio anifungulie. Sikuweza kuita mtu kwa kuwa nyumba ilikuwa self contained na bafu lilikuwa katikati.

Mtoto alishangaa ila nikamdanganya tu, moyoni nilijua ukweli. Hukurudi siku hiyo badala yake ulikuja asubuhi yake na mwanaume, iliniuma sana hata kama dharau sasa ilikuwa too much. Siku ile sitaisahau hata nitapoingia kaburini na kuirudia ardhi ambayo kwayo nilitokana! Nilikuuliza kwanini na kwa sauti ya kilevi ukajibu “kwani we unataka nini” sikujua kasoro zangu kwako na mwanaume wako akakubusu mbele zangu niliumia nikahisi misumari inapigiliwa kwa nyundo kubwa moyoni mwangu. Nilifikiri hata niwapige wote ila nikakumbuka usemi alionisisitizia marehemu baba yangu ya kuwa “Mwanangu usije kuthubutu kufanya maamuzi ukiwa na hasira, bali ichunge hasira yako”

Maisha yangu yalibadilika ghafla, sikuweza kula, hata suruali sasa zilikuwa hazinitoshi kwa kukonda, ulimsahau mtoto na niligeuka mutu wa kumhudumia mtoto, biashara zilianza kufifia. Nilijitahidi kuendesha biashara ila ikashindikana kabisa. Uzito wangu ukapungua kama thuluji iyeyukayo, sasa ulichukua gari na hukurudi nalo. Nilipouliza ulijibu “mali zote ni mimi nimekufundisha kutafta, usinisumbue akili” ilinitesa sana moyo.

Siku ile ukarudi usiku, nilikuwa nimemis sana hata kukukumbatia na kuwa na wewe fargha ukizingatia wewe ndio mke wangu, ilikuwa imepita miezi sijiwa nawe ukisingizia kuchoka mara siku zako. Ni muda mfupi ila nilionja joto la ndoa na kuona ugumu halisi wa ndoa, kweli ndio maana baba alinisisitizia niwe mvumilivu. Nilikua na kiu hasa ya mapenzi ila hukujali hukutaka nikuguse nilijaribu kulazimisha ila nikakata tamaa baada ya kukutana na uchafu wa mwanaume mwenzangu, ndio ilionesha umetoka kutumika mda si mrefu na haukuoga kabisa, nilitoa machozi moyo ukajikunyata kwa machungu niliyokuwa nikiyapitia. Cathe mwanetu alikuwa sasa ameanza kutambua. Alijua hukumpenda tena. Kila siku kwa Janeth hukutaka kushinda nyumbani kabisa. Niligeuka houseboy nilifua nguo za mtoto hata za ndani. Nilikuwa naumia sana, nilifua nguo zako pia hata zile ulizochafua na wanaume wako huko. Moyoni nilijua utabadilika niliamini ni jaribu tu la kupita! Nini kilikubadilisha mke wangu kumbuka tulikotoka. Nilijaribu kukuonya, nikaita ndugu ulikuwa mkali na kwasababu ya pesa ulizo wapa wote waliniona mimi si kitu kabisa ukasingizia mimi ndio mwenye makosa.

Nilishanga siku ukija. Ni kama utani vile ukadai mie na wewe basi. Ukaenda mbali zaidi na kunitambulisha mwanaume eti anakuoa! Sasa niliamini shetani alikushika haswa. Ulichukua hati za nyumba zote ukamkabidhi huyo mwanaume! Niliposema ukanishikia bastola kunipiga, hivi ni kweli nilikuwa adui wako kiasi hicho? Sasa uliniamuru nitoke. Nyumba tulijenga wote ulinifukuza kama mbwa mwizi, na mawanume wako akasema tena kwa daharua
“mchukue na mbwa wako muondoke sisi tule raha” alimwita mwanetu “mbwa” hukustuka mke wangu Jakie badala yake ulimpongeza kwa kumpa busu mubashara! Busu nililoshuhudia lilifanya chozi la kiume lindoke. Ulimtimua mtoto uliyemzaa kwa uchungu kwa matusi ya nguni sitapenda kuyataja.
Niliondoka nikiwa na nguo chache, hukutaka kunipa hata nauli, hata sehemu yalipo maduka yetu uliamuru wauzaji wasinisaidie hakuna aliyenisikiliza, wote waliniona mkosaji. Kwa kuwa sikupenda kuwaambia watu basi walijua kuna amani. Nilitoka na Rambo yangu na mwanangu kwa huzuni kubwa hata hukuwa na hurumila na chozi la mwanao uliyemzaa kwa uchungu. Hatukujua tunakoenda mimi na mwanao Catherine!! ***********************
MIAKA YA SASA.
Kipi kimekusibu? Unataka kuwa na mimi tena? Ulinitesa vile bado unadai kunipenda? Sikuwa tayari na sikujua ni nani alikuonesha huku tunakoishi mimi na mwanao. Nilikuachia jiji ufurahi na wajanja wenzako sasa ulinifuta huku. Umepauka sura, sio tena mke wangu Yule niliyekujua Jakie, ulikuwa umekonda na kukucheki vizuri nilihisi una ujauzito, ulilia kwa uchungu mwanangu Cathe pia alilia baada ya kukutambua kwani sasa alikuwa kakusahau! Ndio ni hakika alikuwa hakukumbuki. Nywele zako zilipauka na mavazi yaliyochoka sana.

Nilitokwa na machozi kukuona uko hivo, sikupenda urudiane tena nami kwani ulishautafuna Moyo wangu. Ulikuwa ukilia ukiomba nikusamehe kuwa ulinikosea. Sikuwa tayari kabisa kukusamehe, nadhani hata angekuwa mtu mwingine asingekusamehe. Mwanangu alilia sana akiomba nikusamehe, nilikuwa katika wakati mgumu. Uliongea kwa msisistizo ukimsihi mwanetu pindi akikua awe na hesihima na ampende mumewe, uliongea hivo na mengine mengi ila haya yalinifanya nikusamehe maneno yako ambayo kila mara yananifanya niyaaandike kwenye kumbukumbu:
Jakie: “Mwanagu Catherine, nilimtenda babako! Alikuwa mwanaume bora kwangu, hakuwahi kunipiga hakunitesa wala kunitukana, alinipa kila kitu, alinisafisha nilipolewa na kujikojolea, mengine siwezi kusema mwanangu wewe bado mdogo. Mamako najutia sana, MARAFIKI wabaya sana, sikujua kama Janeth angeniweka katika taabu hii, alinidangaya na kunifanya niwe mtumwa wa mapenzi nikiwa tumikia kaka zake, nikamdaharua babako. Hapa nilipo mwanangu Catherine mimi ni mgonjwa, wakati wowote nitakufa nina ujazito na gonjwa kuu sina msaada wowote, kazana kusoma Catherine, nyumba iliuzwa na nikafukuzwa kama mbwa. Mwanangu mheshimu babako ni mwanaume shujaa na wakipekee sana katika ulimwengu wa sasa.”

“Mume wangu baba Catherine, nisamehe sana. Nilikukosea sikuwa na hata chembe ya aibu, nilifanya kila kitu ovyoovyo. Ulivumilia kwa kuwa ulinipenda, nakumbuka nilivokutesa mpaka ukawa kilema wa mguu kwaajili yangu. Yote ulionesha kunipenda! Haitoshi Nikaleta wanaume bila aibu mbele zako hakika wewe ni mwanaume imara sana. Nisamehe naomaba nisamehe, nimerudi kuomba unisamehe ili nife salama mimi si wa kuishi tena, kuzimu kunaningoja na hukumu yangu ni nzito. Nimekonda mwili na moyo pia tafadhali nisamehe tu ili nipate amani ya moyo. Siwezi kurudiana nawe, nitakuambukiza ugonjwa, pia kwa jinsi nilivo sisitahili tena kuwa nawe nisamehe sana baba Catherine ””

Maneno hayo yaliniingia akilini, ndio mama Catherine Alimaziliza kuongea na machozi yakamdondoka, mwanume Marc Samuel nilishindwa kuvumilia nililia kilio kikuu na kumkumbatia. Jamani mapenzi yananguvu bado nilimpenda! Nikiwa nimemkumbatia Akaniambia anahisi baridi kali, nilimbeba na kumpeleka chumbani kwangu, alikuwa mwepesi sana kama mtoto mdogo na nilipomuangalia machoni alikuwa anayafumba, nilimlaza vizuri kitandani, alikuwa anatoa machozi huku kafumba macho, ukimya ulitawala sasa hakutingishika kabisa, nilimuita
“Mke wangu Jakie, amka niangalie nimekusmehe! Nakupenda nipo tayari kuwa nawe kwa hali yeyeote ile, na sitakuacha, mwanao Catherine anakupenda na kafurahi kukuona!” Nilimuona mke wangu akijaribu kuinua macho ili anione, alitoa tu machozi ila hakuweza kufumbua macho yake. Alitikisa kichwa kuashiria kukubali na kisha akawa kimya! Nilimshika mkono na alikuwa wa baridi, nilijaribu kushika kifua chake hakuwa na maziwa kama zamani, mapigo ya moyo yalikuwa hayasikiki. Sasa alikuwa hahemi wala kupumua.
Jakie umetuacha mimi na mwanao Catherine pekee yetu. Upumzike kwa amani mke wangu Jakie. Mwanao Catherine anakulilia sana, MOYONI MWANGU BADO UNAISHI. Sitaoa nitamlea tu mwanetu ZAWADI pekee uliyoniachia Rest in Peace Jakie
“Pumzika kwa amani Jakie, tutonana Mungu akipenda siku zetu zikifika Ukomo**********
Ndugu msomaji.
ASANTE KWA KUISOMA, NAAMINI UMEJIFUNZA…..
Kunawakati Tunadanganyika sababu ya MARAFIKI tulio nao, ila kuna siku utajuta kwanini ulimsikiliza rafiki yako, ndio marafiki ni muhmu ila angalia ni nini anakushauri kabla ya kukifanyia kazi maana ipo siku utagundua umepoteza mwezi na utakuwa ukichomwa na jua Kali pasi na kivuli.

www.absalomfreemusic.com

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here